Jumatatu, 12 Agosti 2013

ARSENAL IKO MBIONI KUMNASA KIUNGO WA BAYERN MUNICH

Klabu ya Arsenal yenye maskani yake jijini London, iko mbioni kukamilisha usajili wa kiungo mbrazili Luiz Gustavo kutaka klabu ya Bayern Munich ya Ujerumani. Mchezaji huyo anatarajiwa kutua Emirates kabla ya mechi ya kufungua rasmi pazia la ligi kuu ya Uingereza huku wakicheza na klabu ya Aston villa. Gustavo anaonekana kujihami baada ya usajili wa kiungo wa Barcelona Thiago Alkantara pamoja na kuwepo kwa mkali Bastian Schweinsteiger kwenye klabu ya Bayern Munich, hivyo kuonekana kupoteza nafasi ya kwanza kikosini hapo. Hata ivyo kocha Wenger anataka kurudisha nguvu kwenye nafasi ya kiungo wa kati, nafasi inayochezwa na Mhispania Arteta ambaye kiumri naye muda wake uko mbioni kuisha kisoka, pia kocha huyo anategemea kuziba ufa la Mkameruni Song aliyetimkia Barcelona. Kwa ada ya pauni milioni 14 Wenger anategemea kumnyakua kiungo huyo. Sanogo ndiye mchezaji ambaye mpaka sasa klabu ya Arsenal imemsajili kwa uhamisho huru akitokea nchini Ufaransa. Ikumbukwe kwamba klabu ya Arsenal imeendelea kumnyemelea mshambuliaji wa Liverpool Luis Suares wakatihuohuo ikianzisha tena kumtaka mshambuliaji wa Manchester United Wayne Rooney baada ya klabu ya Chelsea kuonekana kukata tamaa kumnsa mchezaji huyo raia wa Uingereza.