Swansea City wamekubali ada ya uhamisho ya takriban pauni milioni 30 kutoka kwa Manchester City ya kumnunua Wilfried Bony, 26.
Meneja wa Swansea, Gary Monk alisema kuwa itahitaji "kitita cha ajabu" kumhamisha Bony kutoka Swansea.
Alikuwa mfungaji bora wa mwaka wa kalenda 2014 akipachika mabao 20.
Bony alijiunga na Swansea mwaka 2013 akitokea Vitese Arnhem kwa pauni milioni 12.
Mchezaji huyo alifunga bao la kusawazisha katika dakika ya 90 kwenye mechi dhidi ya QPR siku ya mwaka mpya.
Bony kwa sasa yuko na kikosi cha timu ya taifa ya Ivory Coast kujiandaa na michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika.
BANANA MNYOPI BLOG
PATA HABARI MUHIMU KUTOKA VISIWA VYA ZIWA VICTORIA PAMOJA NA HABARI ZA MICHEZO ZA KIMATAIFA

Jumapili, 11 Januari 2015
MCHEZAJI WA WOLFSBURG AFARIKI DUNIA
Kiungo wa klabu ya Wolfsburg ya Ujerumani Junior Malanda, 20, amefariki dunia katika ajali ya gari.
Malanda, aliyekuwa akiichezea timu ya taifa ya Ubelgiji ya chini ya umri wa miaka 21, amecheza mechi 15 msimu huu katika Bundesliga na mechi za Europa League ikiwemo dhidi ya Everton.
Mkurugenzi wa michezo wa Wolfsburg Klaus Allofs amesema katika taarifa: "Tumesikitishwa sana, na hatuamini kilichotokea, hatuna hata maneno ya kusema.
"Hatuamini hayuko nasi tena. Sala zetu katika kipindi hiki kigumu tunazielekeza kwa familia yake."
Allofs ameongeza: "Alikuwa chachu katika timu na mwenye furaha. Junior alikuwa mchezaji kandanda mzuri sana na ambaye ndio kwanza alikuwa akichipukia."
Malanda alihusishwa na kuhamia Fulham na Crystal Palace wakati alipoondoka Zulte Waregem mwaka 2013, lakini badala yake alijiunga na Wolfsburg.
Mchezo wake wa mwisho ulikuwa dhidi ya Cologne waliposhinda 2-1 mwezi Disemba.
Polisi wa Wolfsburg wamesema Malanda alikuwa abiria katika gari lililopata ajali katika barabara kuu karibu na mji wa Bielefeld.
Alikuwa akielekea kuungana na wachezaji wenzake kabla ya kusafiri kwenda Afrika Kusini katika kambi ya mazoezi.

Jumamosi, 10 Januari 2015
LEO JUMAMOSI TETESI ZA SOKA ULAYA - DIRISHA DOGO LA USAJILI
Real Madrid wamewasiliana kwa mara ya kwanza na kipa wa Manchester United David De Gea, kutaka amrithi Iker Casillas. Huenda Real wakatoa pauni milioni, Manchester United watampa David De Gea mshahara wa pauni 140,000 kwa wiki ili asishawishike kwenda Real.
Beki wa Southampton Nathaniel Clyne, 23, ananyatiwa na Manchester United.
Mshambuliaji wa Arsenal Yaya Sanogo, 21, anajiandaa kwenda Crystal Palace kwa mkopo, akikataa kwenda Hull City.
Liverpool wanafikiria kumruhusu kiungo Lucas, 28, kwenda Inter Milan, huku klabu hiyo ya Italy ikitaka kutoa pauni milioni 7 kumnunua.
Tottenham inamnyatia mashambuliaji wa Juventus Sebastian Giovinco, 27.
Sunderland watamruhusu mshambuliaji wao Jozy Altidore, 25, kurejea Marekani mwezi huu, huku timu tatu za MLS zikimtaka.
Leo kimya kidogo- Tetesi nyingine kesho tukijaaliwa. Uhamisho uliotjibitishwa nitakufahamisha utakapothibitishwa. Uwe na Jumamosi njema- Cheers

STERLING APEWA LIKIZO
Mshambuliaji wa Liverpool Raheem Sterling hatokuwepo katika mechi dhidi ya Sunderland siku ya Jumamosi, kwa sababu amepewa mapumziko.
Sterling ambaye yuko mapumzikoni Jamaica ameonesha picha kupitia Instagram akiwa kavaa kofia na miwani.
Boss wa Liverpool Brendan Rodgers amesema alikuwa "amepanga" kumpa likizo mshambuliaji huyo ambaye amecheza dakika nyingi zaidi kuliko mshambuliaji yeyote katika Ligi Kuu ya England msimu huu.

ALEX SONG ASTAAFU SOKA LA KIMATAIFA
Kiungo wa Cameroon na West Ham Alex Song amestaafu kucheza soka la kimataifa baada ya kutotajwa katika kikosi cha timu ya taifa kitakachocheza Kombe la Mataifa ya Afrika. Kiungo huyo, 27, anayecheza kwa mkopo kutoka Barcelona sasa ataweza kuendelea kuichezea West Ham baada ya mazungumzo ya dakika za mwisho na Cameroon kuvunjika. Kupitia Instagram amesema: "Mapenzi yangu kwa nchi yangu hayatobadilika. Nataka kuchukua muda na kuelekeza nguvu zangu kujenga tena fani yangu West Ham United". Song hajaichezea timu yake ya taifa tangu alipopewa kadi nyekundu kwenye mechi dhidi ya Croatia katika ngazi ya makundi katika Kombe la Dunia 2014. West Ham walikuwa na wasiwasi wa kumkosa mchezaji huyo baada ya kwenda Cameroon kujadili uwezekano wa kujumuishwa katika kikosi cha timu ya taifa, kwa ajili ya michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika inayoanza Januari 17 nchini Equatorial Guinea.
Ijumaa, 9 Januari 2015
MOURINHO ASHTAKIWA NA FA
Meneja wa Chelsea Jose Mourinho ameshtakiwa na Chama cha Soka cha England, FA kufuatia madai yake kuwa kuna "kampeni" ya waamuzi dhidi ya timu yake.
Mourinho alitoa matamshi hayo baada ya Chelsea kunyimwa penati dhidi ya Southampton Disemba 28 katika mchezo uliomalizika kwa sare ya 1-1.
Mwamuzi Anthony Taylor alimuonesha kadi ya manjano Cesc Fabegas baada ya kuanguka ndani ya boksi wakati akikabiliwa na Matt Targett.
Mourinho ana hadi Januari 13 kujibu mashtaka hayo.

KIPA WA ARSENAL SZCZESNY AOMBA RADHI
Kipa wa Arsenal Wojciech Szczesny ameomba radhi kwa meneja wake Arsene Wenger, kufuatia taarifa kuwa kipa huyo kutoka Poland alivuta sigara bafuni, baada ya kufungwa 2-0 katika mechi ya siku ya mwaka mpya dhidi ya Southampton. Wenger hakuweza kuthibitisha kuwa Szczesny alikutwa akivuta sigara, lakini amesema mchezaji huyo "alifanya kosa". Lakini Wenger hajasema kama hatomchezesha kipa huyo katika mechi dhidi ya Stoke. "Alifanya makosa, yeye sio wa kwanza, wala wa mwisho," amesema Wenger. "Navutiwa na Wojciech, na akifanya makosa huwajibika.
"Nadhani amechangia mengi katika taswira nzuri ya Arsenal, na anajifunza kutokana na makosa yake.
"Ameomba radhi. Ni kijana makini anayejituma sana." amesema Wenger.

Jisajili kwenye:
Machapisho (Atom)