Jumamosi, 10 Januari 2015

LEO JUMAMOSI TETESI ZA SOKA ULAYA - DIRISHA DOGO LA USAJILI

Real Madrid wamewasiliana kwa mara ya kwanza na kipa wa Manchester United David De Gea, kutaka amrithi Iker Casillas. Huenda Real wakatoa pauni milioni, Manchester United watampa David De Gea mshahara wa pauni 140,000 kwa wiki ili asishawishike kwenda Real.




Beki wa Southampton Nathaniel Clyne, 23, ananyatiwa na Manchester United.

Mshambuliaji wa Arsenal Yaya Sanogo, 21, anajiandaa kwenda Crystal Palace kwa mkopo, akikataa kwenda Hull City.

Liverpool wanafikiria kumruhusu kiungo Lucas, 28, kwenda Inter Milan, huku klabu hiyo ya Italy ikitaka kutoa pauni milioni 7 kumnunua.

Tottenham inamnyatia mashambuliaji wa Juventus Sebastian Giovinco, 27.

Sunderland watamruhusu mshambuliaji wao Jozy Altidore, 25, kurejea Marekani mwezi huu, huku timu tatu za MLS zikimtaka.
Leo kimya kidogo- Tetesi nyingine kesho tukijaaliwa. Uhamisho uliotjibitishwa nitakufahamisha utakapothibitishwa. Uwe na Jumamosi njema- Cheers

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni