Ijumaa, 9 Januari 2015

MOURINHO ASHTAKIWA NA FA

Meneja wa Chelsea Jose Mourinho ameshtakiwa na Chama cha Soka cha England, FA kufuatia madai yake kuwa kuna "kampeni" ya waamuzi dhidi ya timu yake.
Mourinho alitoa matamshi hayo baada ya Chelsea kunyimwa penati dhidi ya Southampton Disemba 28 katika mchezo uliomalizika kwa sare ya 1-1.
Mwamuzi Anthony Taylor alimuonesha kadi ya manjano Cesc Fabegas baada ya kuanguka ndani ya boksi wakati akikabiliwa na Matt Targett.
Mourinho ana hadi Januari 13 kujibu mashtaka hayo.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni