Samatta ambaye yupo nchini kwa mapumziko, amelazimika kufanya hivyo kupisha mkusanyiko wa mashabiki unaokesha nyumbani kwao kwa ajili ya kuomba msaada na wengine wakitaka kumshuhudia tu.
Mwandishi wetu alifika nyumbani kwao na Samatta, Mbagala Rangitatu na kukutana na baba mzazi wa mwanasoka huyo, Ally Samatta aliyeweka wazi kuwa mwanaye yupo jijini, lakini amejificha mahali na huwa anafika nyumbani hapo kwa kuvizia.
Baba huyo alisema awali mwanaye alikuwa akifikia hapo kila alipokuwa anakuja mapumzikoni, lakini hali haikuwa shwari kutokana na watu kujaa hapo mchana na usiku.
“Kila mmoja huja na sababu yake, wengine walikuwa na hamu tu ya kumshuhudia staa huyo na wengine walifika hapo kwa ajili ya kuomba msaada wakijua jamaa amekuja na pesa nyingi kutoka kwa mmiliki wa TP mazembe, Moise Katumbi,” Baba huyo alisema.
“Chumba chake hiko hapo (anakionyesha), lakini sasa hivi hafikii hapa, anafikia huko mbali na anakuja hapa kwa kuvizia tu. Tunawasiliana na akijua nipo anaweza kuja usiku na kukaa masaa mawili matatu na baada ya hapo anaondoka, hata hivyo kwa sababu anatumia gari yake, wanapoiona tu hapo nje ni tabu, wanajaa.
“Kutokana na hali hiyo inanibidi nizoee tu ndiyo hivyo tena, lakini huwa nakosa raha kwa sababu nakosa muda wa kutosha wa kukaa kuzungumza na kufurahia na mwanangu.”

Hata hivyo mchezaji huyo amekiri kuwa anaiheshimu jamii aliyokuwa nayo wakae wazungumze, lakini kutokana na majukumu mengi anayokuwa nayo inambidi afanye hivyo kwa sababu lengo la kuja nyumbani Dar es Salaam ni kupumzisha akili yake.
“Nathamini mchango wa jamii, tukae tuzungumze kama zamani, lakini sasa hivi ni tofauti nina majukumu mengi, hivyo kuna wakati natakiwa nipumzike na ndiyo maana huwa sipatikani kwa urahisi,” alisema Samatta.
Mchezaji huyo pia anaichezea timu ya taifa, Taifa Stars.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni