Ijumaa, 9 Januari 2015

KASENYI HAITAKI UVUVI HARAMU













Hii ni kuonyesha kwamba uvuvi haramu hautakiwi kwa maendeleo ya wavuvi na serikali kwa ujumla, leo kisiwa cha Kasenyi katika kijiji cha Kasenyi na kitongoji cha Kasenyi wameamua kuchoma nyavu haramu aina ya timba, baada ya kuzikamata zikitumika kuvulia samaki kinyume cha sheria ya uvuvi. Kama itaendelea hivi basi angalau maisha ya wavuvi yatabadilika na kuwa maisha yenye neema kwakuwa uvuvi haramu ndio unaopunguza samaki wachanga ziwani na kusababisha kuisha kwa samaki. Maoni yangu kwa kikundi cha kusimamia rasilimali ziwa yaani BMU, hii ishiishie leo tu kwani wako wavuvi wengi saana wanaotumia zana hizi haramu tena wengine ni wanasiasa maarufu hapa kisiwani kwetu. IKIBIDI TUTAANZA KWA KUWATAJA MAJINA. 

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni