Mshambuliaji wa Barcelona Lionel Messi, 27, amesema yuko tayari kuwasikiliza Chelsea au Manchester City, kama timu hizo zitatoa pauni milioni 500 ili kuondoka Spain mwisho wa msimu huu.
Manchester United wanafikiria kutoa pauni milioni 35 kumsajili Mats Hummels, 26, Louis van Gaal akitaka kutumia mwanya wa Borussia Dortmund kusuasua katika Bundesliga msimu huu, hata hivyo van Gaal huenda akalazimika kusubiri hadi mwisho wa msimu kuwasajili Hummels na Kevin Strootman, 24, kutoka Roma, ingawa wachezaji hao wawili wanasema wametulia katika timu zao.
Liverpool wanafikiria kumchukua kipa wa Barcelona Marc-Andre ter Stegen, 22, wakati Brendan Rodgers akitafuta mtu wa kuchukua nafasi ya Simon Mignolet.
Newcastle wanatarajiwa kuzungumza na kocha wa zamani wa Lyon Remi Garde kuchukua nafasi iliyoachwa na Alan Pardew.
Mshambuliaji wa Lyon Alexandre Lacazette, 23, amewapa moyo Arsenal na Liverpool baada ya kusema anataka kucheza Spain au England.
Beki wa Manchester City Matija Nastasic, 21, anakaribia kuhamia Schalke ya Ujerumani siku chache zijazo
Mshambuliaji wa Liverpool, Mario Balotelli, 24, hana nia ya kujiunga na Olympiakos kwa mkopo baada ya timu hiyo ya Ugiriki kujitolea kulipa mshahara wake kamili hadi mwisho wa msimu.
Manchester United itasubiri kuhusu uamuzi wa mkataba mpya wa kipa David De Gea, 24, mpaka mwisho wa msimu, wakati klabu hiyo ikikabiliwa na uamuzi kwanza wa hatma ya Radamel Falcao. De Gea ameahidiwa kupewa pauni 140,000 kwa wiki, ambayo ni mara dufu ya mshahara wake wa sasa ili kuongeza mkataba wake.
Tottenham wanahangaika kuondokana na kiungo Paulinho, 26, kwa sababu si Inter Milan au Schalke zinaweza kutoa pauni milioni 17 zilizolipwa na Spurs kumnunua kutoka Brazil mwaka 2013, lakini Tottenham wanakaribia kukamilisha uhamisho wa mkopo wa Adrien Rabot, 19, kutoka Paris St-Germain.
Meneja wa Aston Vila, Paul Lambert lazima atafute pauni milioni tatu kama atataka kumnunua winga wa Manchester City Scott Sinclair, 25.Wakati huohuo wakala wa Frank Lampard amesema kiungo huyo hatoongeza mkataba wake Manchester City baada ya kumalizika kwa msimu, na atajiunga na New York City mwezi Julai.
shambuliaji wa Liverpool Daniel Sturridge, 25, atarejea mazoezini siku ya Ijumaa baada ya mwezi mzima wa matibabu nchini Marekani.
Tetesi nyingine kesho tukijaaliwa. Habari zilizothibitishwa nitakujulisha, zikithibitishwa. Siku njema! Cheers.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni