Swansea City wamekubali ada ya uhamisho ya takriban pauni milioni 30 kutoka kwa Manchester City ya kumnunua Wilfried Bony, 26.
Meneja wa Swansea, Gary Monk alisema kuwa itahitaji "kitita cha ajabu" kumhamisha Bony kutoka Swansea.
Alikuwa mfungaji bora wa mwaka wa kalenda 2014 akipachika mabao 20.
Bony alijiunga na Swansea mwaka 2013 akitokea Vitese Arnhem kwa pauni milioni 12.
Mchezaji huyo alifunga bao la kusawazisha katika dakika ya 90 kwenye mechi dhidi ya QPR siku ya mwaka mpya.
Bony kwa sasa yuko na kikosi cha timu ya taifa ya Ivory Coast kujiandaa na michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika.
PATA HABARI MUHIMU KUTOKA VISIWA VYA ZIWA VICTORIA PAMOJA NA HABARI ZA MICHEZO ZA KIMATAIFA

Jumapili, 11 Januari 2015
MCHEZAJI WA WOLFSBURG AFARIKI DUNIA
Kiungo wa klabu ya Wolfsburg ya Ujerumani Junior Malanda, 20, amefariki dunia katika ajali ya gari.
Malanda, aliyekuwa akiichezea timu ya taifa ya Ubelgiji ya chini ya umri wa miaka 21, amecheza mechi 15 msimu huu katika Bundesliga na mechi za Europa League ikiwemo dhidi ya Everton.
Mkurugenzi wa michezo wa Wolfsburg Klaus Allofs amesema katika taarifa: "Tumesikitishwa sana, na hatuamini kilichotokea, hatuna hata maneno ya kusema.
"Hatuamini hayuko nasi tena. Sala zetu katika kipindi hiki kigumu tunazielekeza kwa familia yake."
Allofs ameongeza: "Alikuwa chachu katika timu na mwenye furaha. Junior alikuwa mchezaji kandanda mzuri sana na ambaye ndio kwanza alikuwa akichipukia."
Malanda alihusishwa na kuhamia Fulham na Crystal Palace wakati alipoondoka Zulte Waregem mwaka 2013, lakini badala yake alijiunga na Wolfsburg.
Mchezo wake wa mwisho ulikuwa dhidi ya Cologne waliposhinda 2-1 mwezi Disemba.
Polisi wa Wolfsburg wamesema Malanda alikuwa abiria katika gari lililopata ajali katika barabara kuu karibu na mji wa Bielefeld.
Alikuwa akielekea kuungana na wachezaji wenzake kabla ya kusafiri kwenda Afrika Kusini katika kambi ya mazoezi.

Jumamosi, 10 Januari 2015
LEO JUMAMOSI TETESI ZA SOKA ULAYA - DIRISHA DOGO LA USAJILI
Real Madrid wamewasiliana kwa mara ya kwanza na kipa wa Manchester United David De Gea, kutaka amrithi Iker Casillas. Huenda Real wakatoa pauni milioni, Manchester United watampa David De Gea mshahara wa pauni 140,000 kwa wiki ili asishawishike kwenda Real.
Beki wa Southampton Nathaniel Clyne, 23, ananyatiwa na Manchester United.
Mshambuliaji wa Arsenal Yaya Sanogo, 21, anajiandaa kwenda Crystal Palace kwa mkopo, akikataa kwenda Hull City.
Liverpool wanafikiria kumruhusu kiungo Lucas, 28, kwenda Inter Milan, huku klabu hiyo ya Italy ikitaka kutoa pauni milioni 7 kumnunua.
Tottenham inamnyatia mashambuliaji wa Juventus Sebastian Giovinco, 27.
Sunderland watamruhusu mshambuliaji wao Jozy Altidore, 25, kurejea Marekani mwezi huu, huku timu tatu za MLS zikimtaka.
Leo kimya kidogo- Tetesi nyingine kesho tukijaaliwa. Uhamisho uliotjibitishwa nitakufahamisha utakapothibitishwa. Uwe na Jumamosi njema- Cheers

STERLING APEWA LIKIZO
Mshambuliaji wa Liverpool Raheem Sterling hatokuwepo katika mechi dhidi ya Sunderland siku ya Jumamosi, kwa sababu amepewa mapumziko.
Sterling ambaye yuko mapumzikoni Jamaica ameonesha picha kupitia Instagram akiwa kavaa kofia na miwani.
Boss wa Liverpool Brendan Rodgers amesema alikuwa "amepanga" kumpa likizo mshambuliaji huyo ambaye amecheza dakika nyingi zaidi kuliko mshambuliaji yeyote katika Ligi Kuu ya England msimu huu.

ALEX SONG ASTAAFU SOKA LA KIMATAIFA
Kiungo wa Cameroon na West Ham Alex Song amestaafu kucheza soka la kimataifa baada ya kutotajwa katika kikosi cha timu ya taifa kitakachocheza Kombe la Mataifa ya Afrika. Kiungo huyo, 27, anayecheza kwa mkopo kutoka Barcelona sasa ataweza kuendelea kuichezea West Ham baada ya mazungumzo ya dakika za mwisho na Cameroon kuvunjika. Kupitia Instagram amesema: "Mapenzi yangu kwa nchi yangu hayatobadilika. Nataka kuchukua muda na kuelekeza nguvu zangu kujenga tena fani yangu West Ham United". Song hajaichezea timu yake ya taifa tangu alipopewa kadi nyekundu kwenye mechi dhidi ya Croatia katika ngazi ya makundi katika Kombe la Dunia 2014. West Ham walikuwa na wasiwasi wa kumkosa mchezaji huyo baada ya kwenda Cameroon kujadili uwezekano wa kujumuishwa katika kikosi cha timu ya taifa, kwa ajili ya michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika inayoanza Januari 17 nchini Equatorial Guinea.
Ijumaa, 9 Januari 2015
MOURINHO ASHTAKIWA NA FA
Meneja wa Chelsea Jose Mourinho ameshtakiwa na Chama cha Soka cha England, FA kufuatia madai yake kuwa kuna "kampeni" ya waamuzi dhidi ya timu yake.
Mourinho alitoa matamshi hayo baada ya Chelsea kunyimwa penati dhidi ya Southampton Disemba 28 katika mchezo uliomalizika kwa sare ya 1-1.
Mwamuzi Anthony Taylor alimuonesha kadi ya manjano Cesc Fabegas baada ya kuanguka ndani ya boksi wakati akikabiliwa na Matt Targett.
Mourinho ana hadi Januari 13 kujibu mashtaka hayo.

KIPA WA ARSENAL SZCZESNY AOMBA RADHI
Kipa wa Arsenal Wojciech Szczesny ameomba radhi kwa meneja wake Arsene Wenger, kufuatia taarifa kuwa kipa huyo kutoka Poland alivuta sigara bafuni, baada ya kufungwa 2-0 katika mechi ya siku ya mwaka mpya dhidi ya Southampton. Wenger hakuweza kuthibitisha kuwa Szczesny alikutwa akivuta sigara, lakini amesema mchezaji huyo "alifanya kosa". Lakini Wenger hajasema kama hatomchezesha kipa huyo katika mechi dhidi ya Stoke. "Alifanya makosa, yeye sio wa kwanza, wala wa mwisho," amesema Wenger. "Navutiwa na Wojciech, na akifanya makosa huwajibika.
"Nadhani amechangia mengi katika taswira nzuri ya Arsenal, na anajifunza kutokana na makosa yake.
"Ameomba radhi. Ni kijana makini anayejituma sana." amesema Wenger.

KASENYI HAITAKI UVUVI HARAMU
Hii ni kuonyesha kwamba uvuvi haramu hautakiwi kwa maendeleo ya wavuvi na serikali kwa ujumla, leo kisiwa cha Kasenyi katika kijiji cha Kasenyi na kitongoji cha Kasenyi wameamua kuchoma nyavu haramu aina ya timba, baada ya kuzikamata zikitumika kuvulia samaki kinyume cha sheria ya uvuvi. Kama itaendelea hivi basi angalau maisha ya wavuvi yatabadilika na kuwa maisha yenye neema kwakuwa uvuvi haramu ndio unaopunguza samaki wachanga ziwani na kusababisha kuisha kwa samaki. Maoni yangu kwa kikundi cha kusimamia rasilimali ziwa yaani BMU, hii ishiishie leo tu kwani wako wavuvi wengi saana wanaotumia zana hizi haramu tena wengine ni wanasiasa maarufu hapa kisiwani kwetu. IKIBIDI TUTAANZA KWA KUWATAJA MAJINA.
MBWANA SAMATTA AKIMBIA........
KATIKA hali isiyo ya kawaida, staa wa TP Mazembe ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, Mtanzania Mbwana Samatta, amelazimika kuyakimbia kwa muda makazi ya familia yaliyopo jijini Dar es Salaam.
Samatta ambaye yupo nchini kwa mapumziko, amelazimika kufanya hivyo kupisha mkusanyiko wa mashabiki unaokesha nyumbani kwao kwa ajili ya kuomba msaada na wengine wakitaka kumshuhudia tu.
Mwandishi wetu alifika nyumbani kwao na Samatta, Mbagala Rangitatu na kukutana na baba mzazi wa mwanasoka huyo, Ally Samatta aliyeweka wazi kuwa mwanaye yupo jijini, lakini amejificha mahali na huwa anafika nyumbani hapo kwa kuvizia.
Baba huyo alisema awali mwanaye alikuwa akifikia hapo kila alipokuwa anakuja mapumzikoni, lakini hali haikuwa shwari kutokana na watu kujaa hapo mchana na usiku.
“Kila mmoja huja na sababu yake, wengine walikuwa na hamu tu ya kumshuhudia staa huyo na wengine walifika hapo kwa ajili ya kuomba msaada wakijua jamaa amekuja na pesa nyingi kutoka kwa mmiliki wa TP mazembe, Moise Katumbi,” Baba huyo alisema.
“Chumba chake hiko hapo (anakionyesha), lakini sasa hivi hafikii hapa, anafikia huko mbali na anakuja hapa kwa kuvizia tu. Tunawasiliana na akijua nipo anaweza kuja usiku na kukaa masaa mawili matatu na baada ya hapo anaondoka, hata hivyo kwa sababu anatumia gari yake, wanapoiona tu hapo nje ni tabu, wanajaa.
“Kutokana na hali hiyo inanibidi nizoee tu ndiyo hivyo tena, lakini huwa nakosa raha kwa sababu nakosa muda wa kutosha wa kukaa kuzungumza na kufurahia na mwanangu.”

Hata hivyo mchezaji huyo amekiri kuwa anaiheshimu jamii aliyokuwa nayo wakae wazungumze, lakini kutokana na majukumu mengi anayokuwa nayo inambidi afanye hivyo kwa sababu lengo la kuja nyumbani Dar es Salaam ni kupumzisha akili yake.
“Nathamini mchango wa jamii, tukae tuzungumze kama zamani, lakini sasa hivi ni tofauti nina majukumu mengi, hivyo kuna wakati natakiwa nipumzike na ndiyo maana huwa sipatikani kwa urahisi,” alisema Samatta.
Mchezaji huyo pia anaichezea timu ya taifa, Taifa Stars.

HII NI MAALUMU KWA MABAAMEDI
Hizi ni opena mpyaa kabisa za mwaka 2015. Kazo kwenu wateja wa baa, lakini najiuliza swali moja sipati majibu, Ni kwanini wamweka sanamu za namna hii? au ni kwasababu kazi yenyewe inafanana saaana na shughuli hii? Au wewe unasemaje? Kwa wale wenzangu wa kasenyi mkitoka ''doro'' mfike kwa mama mtakuta wahudumu wake wameshilikia mkononi hizo zana. Ila natania tu sijui kama mama ameshaleta OPENA za namna hiyo. Swali kwa wahudumu, ivi ukiwa umeishika opena hiyo unataka kufungulia kinywaji unahisi nini mkononi?
TETESI ZA SOKA ULAYA- DIRISHA DOGO LA USAJILI
Mshambuliaji wa Barcelona Lionel Messi, 27, amesema yuko tayari kuwasikiliza Chelsea au Manchester City, kama timu hizo zitatoa pauni milioni 500 ili kuondoka Spain mwisho wa msimu huu.
Manchester United wanafikiria kutoa pauni milioni 35 kumsajili Mats Hummels, 26, Louis van Gaal akitaka kutumia mwanya wa Borussia Dortmund kusuasua katika Bundesliga msimu huu, hata hivyo van Gaal huenda akalazimika kusubiri hadi mwisho wa msimu kuwasajili Hummels na Kevin Strootman, 24, kutoka Roma, ingawa wachezaji hao wawili wanasema wametulia katika timu zao.
Liverpool wanafikiria kumchukua kipa wa Barcelona Marc-Andre ter Stegen, 22, wakati Brendan Rodgers akitafuta mtu wa kuchukua nafasi ya Simon Mignolet.
Newcastle wanatarajiwa kuzungumza na kocha wa zamani wa Lyon Remi Garde kuchukua nafasi iliyoachwa na Alan Pardew.
Mshambuliaji wa Lyon Alexandre Lacazette, 23, amewapa moyo Arsenal na Liverpool baada ya kusema anataka kucheza Spain au England.
Beki wa Manchester City Matija Nastasic, 21, anakaribia kuhamia Schalke ya Ujerumani siku chache zijazo
Mshambuliaji wa Liverpool, Mario Balotelli, 24, hana nia ya kujiunga na Olympiakos kwa mkopo baada ya timu hiyo ya Ugiriki kujitolea kulipa mshahara wake kamili hadi mwisho wa msimu.
Manchester United itasubiri kuhusu uamuzi wa mkataba mpya wa kipa David De Gea, 24, mpaka mwisho wa msimu, wakati klabu hiyo ikikabiliwa na uamuzi kwanza wa hatma ya Radamel Falcao. De Gea ameahidiwa kupewa pauni 140,000 kwa wiki, ambayo ni mara dufu ya mshahara wake wa sasa ili kuongeza mkataba wake.
Tottenham wanahangaika kuondokana na kiungo Paulinho, 26, kwa sababu si Inter Milan au Schalke zinaweza kutoa pauni milioni 17 zilizolipwa na Spurs kumnunua kutoka Brazil mwaka 2013, lakini Tottenham wanakaribia kukamilisha uhamisho wa mkopo wa Adrien Rabot, 19, kutoka Paris St-Germain.
Meneja wa Aston Vila, Paul Lambert lazima atafute pauni milioni tatu kama atataka kumnunua winga wa Manchester City Scott Sinclair, 25.Wakati huohuo wakala wa Frank Lampard amesema kiungo huyo hatoongeza mkataba wake Manchester City baada ya kumalizika kwa msimu, na atajiunga na New York City mwezi Julai.
shambuliaji wa Liverpool Daniel Sturridge, 25, atarejea mazoezini siku ya Ijumaa baada ya mwezi mzima wa matibabu nchini Marekani.
Tetesi nyingine kesho tukijaaliwa. Habari zilizothibitishwa nitakujulisha, zikithibitishwa. Siku njema! Cheers.

Alhamisi, 8 Januari 2015
BURUDANI YA KASENYI KWETU
Dude hilo limekuja kututembelea Kasenyi. Watu wanatalii bila malipo, lakini huyu mnyama ni moja ya washikaji wetu. Unaweza kuwa na moyo wa ujasiri wa kupiga nalo picha? Ebu angalia washikaji nilivyowapiga picha wakiwa karibu kabisa nalo.
Lakini Smoka likataka kumkimbiza ebu angalia
HIYO NI MOJA YA RAHA YA MALIASILI YA TANZANIA NA RAHA YA KUISHI KISIWANI. KUMBUKA NILIKUWA NIMEIFUNGA BLOGU HII KWA KARIBU MIAKA MIWILI, LAKINI KUANZIA SASA NIKO HEWANI.
Kwa wale wapenzi wa Yanga poleni sana kwa kutolewa kwenye kombe la mapinduzi. Ata mimi mpenzi wa Azam nimeshazoea, sijui Simba wao itakuwaje? Bora kombe libaki Zanzibar!!!!!

Jisajili kwenye:
Machapisho (Atom)