PATA HABARI MUHIMU KUTOKA VISIWA VYA ZIWA VICTORIA PAMOJA NA HABARI ZA MICHEZO ZA KIMATAIFA

Jumanne, 30 Julai 2013
TUWE NA SHUKRANI KWA MOURINHO-CASILLAS
Kapteni wa klabu ya Real Madrid mkongwa Ike Casillas, ameshauri iwepo shukrani kwa aliyekuwa kocha wao Jose Mourinho, mlinda mlango huyo aliyejikuta anapoteza nafasi yake ya kikosi cha kwanza mwishoni mwa msimu uliopita, amesema kocha huyo anayeinoa klabu ya matajiri wa London kwa sasa inabidi apewe heshima yake kwani amefanya makubwa kwa kipindi cha miaka mitatu aliyokaa Santiago Bernabeu. '' Kwa sasa ninafundishwa na kocha mwingine, lakini bado sijaona utofauti wowote'' alitanabaisha mlinda mlango huyo wa timu ya taifa ya Hispania. Miaka mitatu aliyokaa Jose Mourinho ameweza kubeba mataji matatu lakini kuna baadhi ya wadau wa soka wanaobeza kazi aliyoifanya kocha huyo. ''Najua kuwa kuna magolikipa wazuri katika klabu yangu lakini inanibidi niwe na juhudi ili kuwa namba moja'' alisema mkongwe Casillas.
LEWANDOWSKI asema ''NITAWEKA UWEZO WANGU WOTE KWA DORTMUND''
Mchezaji aliyekuwa na misukosuko katika kipindi hiki cha usajili Robert Lewandowski wa klabu ya nchini Ujerumani ya Borrusia Dortmund, amesema yuko tayari kucheza kwa kiwango chake chote katika klabu yake hiyo. Mchezaji huyo aliyekuwa ameamua kuihama klabu yake kutimukia klabu ya Bayern Munich, alikutana na vikwazo kibao kutoka kwenye klabu yake na kuishia kushindwa kutimiza lengo lake la kuhama. Baada ya kucheza mchezo wa SUPER CUP, Borrusia Dortmund iliishinda klabu ya Bayern Munich kwa goli 4-2, baada ya mchezo huo, mchezaji huyo raia wa Polandi alisema ameamua kurudisha mapenzi yake kwa Dortmund kwani alikwisha poteza mahusiano ya karibu hata na wachezaji wenzake klabuni humo. '' Niko tayari kushinda mataji mengine zaidi ya hili (super cup) nikiwa na klabu yangu ya Borrusia Dortmund'' alisema mchezaji huyo.
SITAKI KWENDA MAN U, NATAKA KUBAKI BARCA
Kocha David Moyes wa Man U anaonekana kuangukia pua kwa lengo lake la kumsajili kiungo mchezeshaji raia wa Hispania Cesc Fabregas, kiungo huyo alikuwa ndo chagua la kwanza katika dirisha la usajili msimu huu kwa kocha mpya wa Man U. Moyes alikuwa tayari ameshatenga kiasi cha paundi milioni 35 kwa ajili ya ada ya kumsajili kijana huyo. Kitendo cha mchezaji huyu mwenye umri wa miaka 26 kutamka kwamba atasalia kwenye klabu yake bingwa wa ligi mwaka huu. Mchezaji huyo amenukuliwa akiwaambia marafiki zake kwamba watakuwa wote Camp nou msimu ujao na anapenda kuendelea kusakata kabumbu kwenye klabu ya Barcelona msimu huu. Inaonekana kwamba baada ya Moyes kumkosa kiungo huyo, sasa amehamishia nguvu zake kwa kiungo wa zamani wa klabu ya Tottenham aliyeko klabu ya Real Madrid Luka Modric pia ametenga kiasi cha yuro milioni 25 ili kumnasa kiungo aliyekuwa naye kwenye klabu ya Everton mbeligiji Marouane Fellaini ambaye analipwa na klabu yake ya sasa kiasi cha yuro 87,000 kwa wiki.
NEYMAR KUWA KIKOSINI BARCA DHIDI YA LECHIA GDANSK
Mchezaji aliyehamia klabu ya Barcelona akitokea klabu ya Santos ya nchini Brazil ataoinekana kwenye kikosi cha Barca kwenye mechi ya kirafiki dhidi ya klabu ya Lechia gdansk, mchezaji huyo raia wa Brazil alionekana kuwa mwiba kwenye mashindano ya shirikisho yaliyomalizika mwezi jana huko Brazil.
TUTAMUUZA BALE KAMA TU WATAFIKA BEI
Klabu ya Tottenham imekubali kumuuza mchezaji wake mwenyekuonekana kuwa tishio kwa sasa kama tu timu inayomuwania itakuwa tayari kutoa kiasi cha paundi milioni 85 na mchezaji mmoja. Klabu tajiri ya Real Madrid ndiyo inayomsaka kijana huyo mwenye umri wa miaka 23 kwa udi na uvumba. Ikumbukwe pale jana Madrid walitoa ofa ya wachezaji wawili pamoja na kitita cha paundi milioni 53 ili kumnasa mchezaji huyo rai wa Wales. Hata ivyo mchezaji huyo aliomba kuongea na klabu ya Madrid kabla hawajafanya chochote juu ya mauziano hayo. Kauli hiyo imetolewa baada ya kuona kwamba klabu ya Real Madrid imedhamiria kumnasa kijana huyo.
Jumatatu, 29 Julai 2013
MAN UNITED YAMTAKA KIUNGO LUKA MODRIC......
Kocha wa klabu ya Man United David Moyes, amehamishia nguvu zake kwa kumtaka kiungo wa klabu ya Real Madrid Luka Modric. Inaonekana kwamba kocha huyo aliyechukua mikoba ya Mscoti mwenzie Alex Furgerson, anataka kuimarisha safu ya kiungo kwenye timu yake hiyo mpya. Baada ya kumtaka bila mafanikio kiungo wa Barcelona Cesc Fabregas kocha huyo amejiandaa kutoa kitita cha paundi milioni 25 kama ada ua uhamisha wa mchezaji huyo.
Ijumaa, 26 Julai 2013
BARCELONA YAANDAA MILIONI 29 KWA DAVID LUIZ
Klabu ya Barcelona imejipanga kuimarisha safu yake ya ulinzi kwa kumfukuzia mlinzi hatari wa klabu ya Chelsea ya Uingereza. Baada ya kukataliwa na klabu ya PSG kwa kumtaka mlinzi wake hatari raia wa Brazil Thiago Silva, klabu hiyo imehamishia nguvu zake kwa mbrazili mwingine huyu Davud Luiz baada ya kuona hana nafasi kubwa kwa kocha mreno Jose Mourinho. Kocha Mourinho hapendezwi sana na staili ya ukabaji wa Luiz ambaye alitua darajani hapo mwaka 2011 akitokea klabu ya Benfica ya Ureno, hata ivyo mbrazili huyo mwenye umri wa miaka 26 alikuwa chagua la kwanza mwaka jana kwa kocha Rafael Bernitez aliyekuwa akikifundisha kikosi hicho cha matajiri wa jiji la London kabla ya kutimukia Italia kwenye klabu yake ya sasa ya Napoli. Jose Mourinho yuko tayari kumuuza Luiz na pesa zake kumnunua mbrazili mwingine kinda mwenye umri wa miaka 18 Doria anayekipiga katika klabu ya Botafogo. Barcelona wanajipanga kuimarisha safu yao ya ulinzi, na baadhi ya walinzi wanaowawania ni pea kutoka Arsenal Laurent Koscielny na mwenzie Thomas Vermaelen, na pia walikuwa wametoa ofa ya yuro milioni 20 kwa mlinzi wa klabu ya Roma Marquinhos kabla ya kuzidiwa kete na matajiri wa Ufaransa klabu ya PSG.BARCELONA YAMTAMBULISHA MARTINO RASMI....
Mabingwa wa ligi ya Hispania klabu ya Barcelona, leo imemtambulisha rasmi muajentiana Gerardo Martino mbele ya mashabiki wao katika uwanja wake wa Camp Nou kuwa ndiye anayechukuwa nafasi ya Tito Villanova ambaye hali yake ya kiafya imemfanya kupumzika kazi hiyo ili arejee kwenye matibabu. Tito Villanova alichukuwa mikoba ya aiyekuwa kocha wake mkuu Pep Guardiola mwenye umri wa miaka 42, aliyeamua kuacha kazi na kupumzika kufundisha soka kwa mwaka mmoja kabla ya kujiunga na mabingwa wa ulaya klabu ya Bayern Munich ya Ujerumani. Tito Villanova hali yake kiafya ilibadilika mwishoni mwa mwaka jana na kuiacha klabu yake chini ya msaidizi wake. Hata ivyo mwanzoni mwa mwezi wa 6 mwaka huu, hali yake ilirudia kuwa mbaya na hatimaye mwanzoni mwa mwezi wa 7 ilibidi akubali kuacha kazi kwa ajili ya afya yake. Ndipo klabu ya Barcelona ilipochukua jukumu la kutafuta kocha atakayeweza kuiendeleza kazi ya Tito Villanova. Muajentina Gerardo Martino ndiye aliyefanikiwa kuchukua nafasi hiyo. Martino hajawahi kufundisha klabu yeyote ya Ulaya, ametokea klabu ya Newell Old Boy ya Ajentina na alishawahi kufundisha timu ya taifa ya Paraguai kwa miaka kadhaa. Ikumbukwe kwamba mshambuliaji Lionel Messi kabla ya kuichezea klabu ya Barcelona, alikuw ni mchezaji wa klabu aliyotoka kocha huyo Martino ya Newell old Boy kuanzia mwaka 1995 mpaka 2000 alipojiunga na klabu ya Barcelona, wachambuzi wengi wa soka wanamtaja kocha huyo kwamba si mzoefu wa soka la Ulaya, lakini mchezaji wa Barcelona Jarvier Marscherano ambaye naye ni raia wa Ajentina anabeza maneno hayo kwa kumtetea muajentina mwenzake kwamba ''hajawahi kunifundisha, lakini ni kocha mzuri ameweza hata kuibadilisha klabu ya Newell Old Boys'' hata ivyo mchezaji huyo alisema ingawa kila kocha huja na mfumo wake wa ufundishaji wake, lakini timu yetu haibadiliki kimfumo.
HATUMUUZI FABREGAS KWA BEI YEYOTE..........
Mabingwa wa ligi ya Hispania klabu ya Barcelona wameiambia klabu ya Manchester United kwamba hawajisikii kumuuza kiungo mchezeshaji wa Cecs Fabregas kwa garama yeyote. Kupitia kwa makamu raisi wa klabu hiyo Josep Maria Bartomeu amesema klabu hiyo haijawa tayari kumuuza kiungo huyo aliyesajiliwa misimu miwili iliyopita akitokea klabu ya Arsenal nayo ya nchini Uingereza, pia kocha mpya aliyechukua nafasi ya Tito Villanova naye amekazia kauli hiyo kwa kusema ''namuandaa Cesc kuwa kiungo tegemezi'' alisema Muajentina Gerardo Martino ambaye ndiye kocha aliyepewa kazi ya kuinoa klabu hiyo yenye maskani yake Catalani. Ikumbukwa kwamba klabu ya Manchester United imeshajitutumua kwa kutangaza dau la yuro milioni 41 ili kumnasa mchezaji huyo. Kocha David Moyes anaonekana kuvutiwa sana na uchezaji wa Fabregas, lakini majibu yanatatanisha ''Ni kweli Cesc ni mchezaji mzuri sana, lakini HATUKO TAYARI KUMUUZA'' alisema Bartomeu.
TOTTENHAM YAKAMILISHA USAJILI WA CHADLI Klabu ya Tottenham ya nchini Uingereza, imekamilisha usajili wa mchezaji kutoka Twente aitwaye Nacer Chadli, mchezaji huyo raia wa Ubeligiji alifunga magoli 12 msimu uliopita akiwa na klabu yake alikotoka. Anakuwa mchezaji wa pili kusajiliwa na klabu hiyo ya London baada ya kumsajili kiungo mbrazili Paulinho kwa ada ya uhamisho ya yuro milioni 20.
Alhamisi, 25 Julai 2013
CHELSEA WAUA............................
Timu ya soka ya Chelsea imefanya kufuru baada ya kuichabanga goli 8-1 timu yenye wachezaji mchanganyiko wa nchini Indonesia, aliyefungulia mlango wa kufuru hiyo ni mchezaji anayelipwa pesa nyingi kuliko mchezaji yeyote kweny klabu hiyo Eden Harzad kwa mkwaju wa penati dakika ya 21, wachezaji Ramires na Lukaku wametupia mara mbili kwenye kufuru hiyo. Wengine waliofunga ni kama inavyojieleza, Ba (31), Terry (45+1), Traore (50)
WAKATI HUOHUO....................
Wachezaji Juan Mata na Torres, huenda wakakosa mchezo wa kufungua ligi ya Uingereza kutokana na kukabiliwa na majukumu ya timu yao ya taifa ya Hispania, timu ya taifa ya Hispania itakuwa na mchezo wa kupimana nguvu siku tatu kabla ya mechi ya kuanza ligi kuu ya Uingereza.
Jumatano, 24 Julai 2013
NATAKA KUHAMIA ARSENAL asema SUAREZ Mshambuliaji hatari wa klabu ya liverpool Luis Suarez amesema yuko tayari kuilazimisha klabu yake kumpa uhamisho ili ajiunge na klabu ya Arsenal. Mchezaji huyo ambaye mkataba wake unamruhusu kufanya hivyo kama tu timu itakayomtaka itaweza kufikia kiasi cha yuro milion 45.6, ameamua kutamka hayo baada ya klabu ya Arsenal kuwa tayari kulipa kias cha yuro milioni 49 kama ada ya uhamisho kwa mchezaji huyo lakini kocha wake amekataa kukubali kiasi hicho cha fedha akidai kwamba Suarez ana thamani sawa na mshambuliaji wa PSG Edson Cavani yaani yuro milioni 63 alizonunuliwa kutoka klabu ya Napoli ya Italia wiki iliyopita. Hata ivyo mshambuliaji huyo wa Liverpool amecheza mechi ya kupimana nguvu akitokea benchi na kutoa pasi ya goli la pili na la ushindi kwa timu hiyo. Suarez amesema ataiandikia Liverpool ili ilazimike kumuuza mchezaji huyo huku klabu ya Arsenal tayari ikijiamini kuwa ndiyo inategemea kumpata mshambuliaji huyo wakati wowote. Lakini wachambuzi wengi wa soka watashangaa sana iwapo klabu ya Arsenal itafanikiwa kumnasa mchezaji huyo kwani hapo awali alishaviponda vyombo vya habari vya Uingereza akidai vinamuharibia maisha yake hapo Uingereza kwahiyo hatokuwa tayari kusalia nchini humo. Ikumbukwe kwamba pia klabu kongwe ya nchini Hispania nayo inamuhitaji mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 26 raia wa Uruguai.
NDOTO ZA ARSENAL KUMSAJILI HIGUAN ZAFIKIA MWISHO........... Klabu ya Napoli ya Italia imekubaliana na mshambuliaji wa Real Madrid Gonzalo Higuan kumlipa kiasi cha yuro 163,000 kwa wiki hii ikiwa ni baada ya makubaliano kati ya vilabu hivi viwili kukubaliana ada ya uhamisho kiasi cha yuro milion 37. Mchezaji huyo atasaini mkataba wa miaka 5 wenye thamani ya yuro milioni 42.3 kwa mshahara wa miaka 5 tu. Ikumbukwe kwamba klabu ya Arsenal ndiyo walionekana kuwa na nafasi kubwa ya kumnasa mshambuliaji huyo raia wa Ajentina, lakini walishindwa kuafikiana ada ya uhamisho wa mshambuliaji huyo. Arsenal walikwisha kubaliana na Higuan mwenyewe lakini wakashindwa kufikia dau la yuro milioni 30 ambalo Real Madrid walitaka kama ada ya uhamisho. Kwa sasa klabu ya washika bunduki wa London wamehamishia nguvu zao kwa mshambuliaji wa kimataifa wa Uruguai Luis Suarez, ambapo mpaka sasa wako tayari kulipa ada ya uhamisho wa mchezaji huyo kiasi cha yuro milioni 49, hata hivyo klabu inayommiliki haijawa tayari kupokea kitita hicho.
KLABU YA VALENCIA IKO TAYARI KUMUUZA MSHAMBULIAJI WAKE SOLDADO KWA TOTTENHAM.... Klabu ya Valencia ya nchini Hispania iko tayari kumuuza mshambuliaji wake hatari Soldado kwa timu ya Uingereza kama tu watafikia kiwango cha ada ya uamisho kiasi cha Yuro milioni 30 sawa na paundi milioni26, kwa muda mrefu sasa klabu ya Tottenham imekuwa ikimuwania mchezaji huyo wa kimataifa wa Hispania. Raisi wa klabu ya Valencia Amadeo Salvo amesema wako tayari kumruhusu mchezaji huyo kuhama kama tu timu inayomtataka itafika dau hilo. Mtaalamu wa benchi la ufundi kutoka klabu ya Tottenham Flanco Baldini alikwenda nchini Hispania ili kumaliza suala la kumnasa mshambuliaji huyo, lakini klabu hiyo ilikataa kupunguza dau hilo. ''hatukuwa na mpango wa kumuuza mshambuliaji wetu huyu, lakini kama mtafika dau hatunabudi kumuuza'' alisema rais wa klabu ya Valencia.
Kocha Villa Boas akiongea na waandishi wa habari wa Hong Kong alisema wanahitaji huduma ya mshambuliaji huyo mwenye umri wa miak 28.
KLABU YA CHELSEA YAKATAA KUMUUZA MATA.....
Klabu ya matajiri wa London Chelsea, imepuuza maneno yanayosemwa kwamba inataka kumuuza mchezaji wake Juan Mata. Kumekuwa na tetesi kuwa mchezaji huyo atauzwa kwa klabu ya Barcelona au atawekwa kwenye mauziano kwa mabadilishano na mchezaji hatari wa Manchester United Wayne Rooney. Kwa msisitizo zaidi klabu hiyo ya darajani imeamua kuandaa mkataba mnono ili kumuongezea mshahara mchezaji huyo kutoka paundi 70,000 kwa wiki mpaka 100,000 kwa wiki, mkataba utakaomkalisha darajani mpaka mwaka 2018. Mchezaji huyo aliyetua darajani miaka 2 iliyopita akitokea Hispania kwenye klabu ya Valencia, alionekana kutokuwa kipenzi cha kocha Jose Mourinho.
WAKATI HUOHUO ................................
Kocha mwenye maneno mengi, Jose Mourinho amesema yuko tayari kuisaidia timu ya taifa ya Uingereza ili ifanikiwe kufuzu fainali za kombe la dunia zitakazofanyika nchini Brazil mwakani. ''Nitawaandaa wachezaji wangu wa Uingereza ili wawe vizuri kwa ajili ya kuiweka timu yao kwenye mazingira mazuri ya kushiriki kombe la dunia mwakani'' alisema Mourinho, kocha huyo anayependa kuongea mara kwa mara ametaabanisha kwamba wachezaji wake raia wa Uingereza atawapa nafasi kikosini ili wapate uzoefu zaidi.
KATIKA HALI NYINGINE...................
Mreno Jose Mourinho ametanabaisha kwamba klabu yake ya Chelsea haiko kwenye shinikizo kubwa la kutwaa ubingwa msimu huu kama walivyo Manchester City, ''wenzangu wamekwishatumia zaidi ya paundi milioni 100 kwenye usajili ili wabebe kombe'' alisema mwalimu huyo na kusema timu yenye kikosi bora kwa aonavyo yeye ni kikosi cha Pellegrini.
Jumanne, 23 Julai 2013
ARSENAL YAONGEZA KITITA KUMNASA SUAREZ mil 49!
Klabu ya Arsenal ya jijini London, imeamua kupandisha dau lake ili kumnasa mshambuliaji hatari wa klabu ya Liverpool Luiz Suarez. Baada ya kuonekana kuzidiwa kete kwenye soko la wachezaji jioni hii baada ya mchezaji aliyetegenewa kutua kwenye viwanja vya Emirates muajentina Higuan kukaribia kabisa kumwaga wino kwenye klabu ya Napoli ya Italia, washika mtutu hao wa London wameamua kutoa dau la kiasi cha Yuro milion 49 ili kuipata huduma ya mshambuliaji kutoka Uruguai kijana machachari Luis Suarez. Ikionekana kabisa kuwa imedhamiria kumchukua mchezaji huo, klabu ya Arsenal imepanda dau hilo ili kumshawishi mshambuliaji huyo kuona kwamba haikuwa inatania pale ilipotangaza dau la Yuro milion 30 awamu ya kwanza kabla ya kutupiliwa mbali kabisa na Liverpool, hata ivyo klabu ya Liverpool haiko tayari kumuuza mchezaji huyo kwa dau ambalo haitarizika nalo. Ikumbukwe kwamba kocha wa Liverpool amekwisha tamka kwamba mchezaji wake huyo ana thamani sawa na aliyekuwa mshambuliaji wa Napoli Edsoni Cavani ambaye amenunuliwa na klabu ya PSG ya Ufaransa kwa kitita cha Yuro milioni 63, hivyo kufanya mbio za mfaransa Arsene Wenger kuwa ngumu kumpata mshambuliaji huyo ambaye bado anatumukia adhabu ya kukosa mechi 6 za mwanzoni mwa ligi kuu ya Uingereza. Hata ivyo mshambuliaji huyo a meshaonyesha nia ya kuihama klabu hiyo ili acheze katika mashindano ya vilabu bingwa barani ulaya. Katika mkataba wake wa awali, unaonyesha Suarez anaruhusiwa kuhama pale tu klabu itakayomtaka ikifika dau la Yuro milioni 46.5, lakini kocha wa Liverpool amesema hatokuwa tayari kupelekeshwa na mchezaji huyo ili amuuze. Ikumbukwe kuwa klabu tajiri duniani ya Real Madrid nayo inamnyemelea kwa karibu kabisa kijana huyo mwenye umri wa miaka 26.WAKATI HUOHUO
Raisi wa klabu kongwe ya Real Madrid Florentino Perez ametangaza kuwa hajapokea ofa yoyote ya kumtaka mchezaji Christian Ronaldo lakini ametanabaisha kwamba mchezaji huyo atastaafu akiichezea klabu hiyo tajiri duniani, pamoja na tetesi nyingi zinazomhusisha Ronaldo kurudi klabu yake ya zamani ya Manchester United pamoja na matajiri wa PSG kuonekana kumtaka kwa udi na uvumba, Perez amesema winga huyo mwenye umri wa miaka 28 atastaafu soka akiichezea Real Madrid ya nchini Hispania.
CHELSEA WASAJILI KINDA KUTOKA CHILE Klabu ya Chelsea yenye makazi yake katika jiji la London, imemsajili kinda mwenye umri wa miaka 18 kutoka kwenye klabu iitwayo O'Higgns ya nchini Chile, Christian Cuevas ni mchezaji mwenye uwezo wa kucheza kama beki wa kushoto na winga wa kushoto, ameshiriki katika mashindano ya kombe la dunia kwa vijana wenye umri wa chini ya miaka 20 yaliyomalizika hivi karibuni, mchezaji huyu ambaye anakuwa wa nne kusajiliwa msimu huu, amesaini mkataba utakaomkalisaha darajani mpaka mwaka 2018. Wachezaji wengine ambao tayari wamekwisha mwaga wino kwenye klabu hii tajiri ni Andre Schurrle kutoka Bayer Leverkusen, Marco Van Ginkel kutoka Vitesse na mchezaji huru Mark Schwarzer
PATA HABARI MUHIMU ZA TETESI ZA USAJILI KWENYE LIGI MBALIMBALI HUKO MAJUU
Klabu ya Napoli ya nchini italia, imekubaliana na waliokuwa mabingwa wa ligi ya Uhispania mwaka jana klabu ya Real Madrid, kulipa kiasi cha Yuro milioni 37 ili kumsajili mshambuliaji raia wa Ajentina Gonzalo Higuani. Mchezaji huyo ambaye anasakwa wa udi na uvumba na klabu ya Arsenal, bado hajakubaliana na klabu hiyo kongwe ya Italia. Pamoja na makubaliano hayo kati ya timu mbili hizo, Higuani tayari ameshakubaliana na klabu ya Arsenal kila kitu ikiwamo mshahara wa mchezaji huyo. Higuan ambaye analipwa kiasi cha Yuro 75 elfu kwa wiki katika klabu yake ya sasa, amekubaliana na Arsenal kulipwa kiasi cha Yuro 116,000/= kwa wiki, ikiwa ni msahara wa kuanzia, hata ivyo klabu ya Napoli nayo iko tayari kumlipa mchezaji huyo kiasi hicha cha mshahara. Tatizo linaonekana kutokubaliana kwa malipo ya kumnunua mchezaji huyo kati ya timu ya Arsenal na timu ya Real Madrid. Napoli inasaka mshambuliaji wa kati baada ya kumuuza mchezaji wao Cavani kwa matajiri wa Ufaransa klabu ya P.S.G. Hata ivyo Higuan bado ana mkataba wa miaka 2 na timu yake hiyo.
Klabu ya Arsenal ya jijini London, iko katika wakati mzuri wa kumsajili kiungo mchezeshaji kutoka katika timu ya Atletico Mineiro. Mblazili Bernad ambaye anatajwa kutakwa na vilabu vingi kama Tottenham, Liverpool, Borussia Dortmund pamoja na Shakhtar Donetsk, tayari amekwishakubaliana na klabu ya Arsenal kumlipa mshahara wa paund 50,000/ kwa wikina ada kutoka kwenye klabu yake kiasi cha paund milion 21, mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 20, ana uwezo wa kucheza kama kiungo mchezeshaji na winga. Timu ya Arsenal imechangwanywa na soko la wachezaji kutokana na jinsi ambavyo linaendelea. WAKATI HUOHUO klabu ya Arsenal inajiandaa kuongeza dau ili kujaribu kuishawishi klabu ya Liverpool kuwauzia mshambuliaji wao hata Luis Suarez, mchezaji huyo ameonyesha kuwa tayari kujiunga na klabu hiyo ya London ili acheze ligi kuu ya mabingwa msimu huu.
Jumatano, 10 Julai 2013
KISIWA KINACHOTEMBEA NDANI YA ZIWA VICTORIA
Ni kisiwa ambacho kinatembea chenye uwezo wa kubeba hata watu 50 kwa wakati mmoja, kisiwa hiki ambacho kinasadikika kutokea kisiwa cha hifadhi ya taifa ya RUBONDO mkoani GEITA, kwa sasa kimefika katika kisiwa cha Kasenyi-Ikuza.
HAYA NI MAAJABU YA MUNGU KATIKA ZIWA VICTORIA. UNGANA NA BLOG HII KWA TAARIFA ZAIDI KUTOKA VISIWA VILIVYOKO NDANI YA ZIWA VICTORIA.
HAYA NI MAAJABU YA MUNGU KATIKA ZIWA VICTORIA. UNGANA NA BLOG HII KWA TAARIFA ZAIDI KUTOKA VISIWA VILIVYOKO NDANI YA ZIWA VICTORIA.
Jisajili kwenye:
Machapisho (Atom)