PATA HABARI MUHIMU KUTOKA VISIWA VYA ZIWA VICTORIA PAMOJA NA HABARI ZA MICHEZO ZA KIMATAIFA
Ijumaa, 26 Julai 2013
BARCELONA YAANDAA MILIONI 29 KWA DAVID LUIZ
Klabu ya Barcelona imejipanga kuimarisha safu yake ya ulinzi kwa kumfukuzia mlinzi hatari wa klabu ya Chelsea ya Uingereza. Baada ya kukataliwa na klabu ya PSG kwa kumtaka mlinzi wake hatari raia wa Brazil Thiago Silva, klabu hiyo imehamishia nguvu zake kwa mbrazili mwingine huyu Davud Luiz baada ya kuona hana nafasi kubwa kwa kocha mreno Jose Mourinho. Kocha Mourinho hapendezwi sana na staili ya ukabaji wa Luiz ambaye alitua darajani hapo mwaka 2011 akitokea klabu ya Benfica ya Ureno, hata ivyo mbrazili huyo mwenye umri wa miaka 26 alikuwa chagua la kwanza mwaka jana kwa kocha Rafael Bernitez aliyekuwa akikifundisha kikosi hicho cha matajiri wa jiji la London kabla ya kutimukia Italia kwenye klabu yake ya sasa ya Napoli. Jose Mourinho yuko tayari kumuuza Luiz na pesa zake kumnunua mbrazili mwingine kinda mwenye umri wa miaka 18 Doria anayekipiga katika klabu ya Botafogo. Barcelona wanajipanga kuimarisha safu yao ya ulinzi, na baadhi ya walinzi wanaowawania ni pea kutoka Arsenal Laurent Koscielny na mwenzie Thomas Vermaelen, na pia walikuwa wametoa ofa ya yuro milioni 20 kwa mlinzi wa klabu ya Roma Marquinhos kabla ya kuzidiwa kete na matajiri wa Ufaransa klabu ya PSG.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni