PATA HABARI MUHIMU KUTOKA VISIWA VYA ZIWA VICTORIA PAMOJA NA HABARI ZA MICHEZO ZA KIMATAIFA
Ijumaa, 26 Julai 2013
BARCELONA YAMTAMBULISHA MARTINO RASMI....
Mabingwa wa ligi ya Hispania klabu ya Barcelona, leo imemtambulisha rasmi muajentiana Gerardo Martino mbele ya mashabiki wao katika uwanja wake wa Camp Nou kuwa ndiye anayechukuwa nafasi ya Tito Villanova ambaye hali yake ya kiafya imemfanya kupumzika kazi hiyo ili arejee kwenye matibabu. Tito Villanova alichukuwa mikoba ya aiyekuwa kocha wake mkuu Pep Guardiola mwenye umri wa miaka 42, aliyeamua kuacha kazi na kupumzika kufundisha soka kwa mwaka mmoja kabla ya kujiunga na mabingwa wa ulaya klabu ya Bayern Munich ya Ujerumani. Tito Villanova hali yake kiafya ilibadilika mwishoni mwa mwaka jana na kuiacha klabu yake chini ya msaidizi wake. Hata ivyo mwanzoni mwa mwezi wa 6 mwaka huu, hali yake ilirudia kuwa mbaya na hatimaye mwanzoni mwa mwezi wa 7 ilibidi akubali kuacha kazi kwa ajili ya afya yake. Ndipo klabu ya Barcelona ilipochukua jukumu la kutafuta kocha atakayeweza kuiendeleza kazi ya Tito Villanova. Muajentina Gerardo Martino ndiye aliyefanikiwa kuchukua nafasi hiyo. Martino hajawahi kufundisha klabu yeyote ya Ulaya, ametokea klabu ya Newell Old Boy ya Ajentina na alishawahi kufundisha timu ya taifa ya Paraguai kwa miaka kadhaa. Ikumbukwe kwamba mshambuliaji Lionel Messi kabla ya kuichezea klabu ya Barcelona, alikuw ni mchezaji wa klabu aliyotoka kocha huyo Martino ya Newell old Boy kuanzia mwaka 1995 mpaka 2000 alipojiunga na klabu ya Barcelona, wachambuzi wengi wa soka wanamtaja kocha huyo kwamba si mzoefu wa soka la Ulaya, lakini mchezaji wa Barcelona Jarvier Marscherano ambaye naye ni raia wa Ajentina anabeza maneno hayo kwa kumtetea muajentina mwenzake kwamba ''hajawahi kunifundisha, lakini ni kocha mzuri ameweza hata kuibadilisha klabu ya Newell Old Boys'' hata ivyo mchezaji huyo alisema ingawa kila kocha huja na mfumo wake wa ufundishaji wake, lakini timu yetu haibadiliki kimfumo.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni