Ijumaa, 26 Julai 2013

HATUMUUZI FABREGAS KWA BEI YEYOTE..........

Mabingwa wa ligi ya Hispania klabu ya Barcelona wameiambia klabu ya Manchester United kwamba hawajisikii kumuuza kiungo mchezeshaji wa Cecs Fabregas kwa garama yeyote. Kupitia kwa makamu raisi wa klabu hiyo Josep Maria Bartomeu amesema klabu hiyo haijawa tayari kumuuza kiungo huyo aliyesajiliwa misimu miwili iliyopita akitokea klabu ya Arsenal nayo ya nchini Uingereza, pia kocha mpya aliyechukua nafasi ya Tito Villanova naye amekazia kauli hiyo kwa kusema ''namuandaa Cesc kuwa kiungo tegemezi'' alisema Muajentina Gerardo  Martino ambaye ndiye kocha aliyepewa kazi ya kuinoa klabu hiyo yenye maskani yake Catalani. Ikumbukwa kwamba klabu ya Manchester United imeshajitutumua kwa kutangaza dau la yuro milioni 41 ili kumnasa mchezaji huyo. Kocha David Moyes anaonekana kuvutiwa sana na uchezaji wa Fabregas, lakini majibu yanatatanisha ''Ni kweli Cesc ni mchezaji mzuri sana, lakini HATUKO TAYARI KUMUUZA'' alisema Bartomeu.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni