Alhamisi, 25 Julai 2013

CHELSEA WAUA............................

Timu ya soka ya Chelsea imefanya kufuru baada ya kuichabanga goli 8-1 timu yenye wachezaji mchanganyiko wa nchini Indonesia, aliyefungulia mlango wa kufuru hiyo ni mchezaji anayelipwa pesa nyingi kuliko mchezaji yeyote kweny klabu hiyo Eden Harzad kwa mkwaju wa penati dakika ya 21, wachezaji Ramires na  Lukaku wametupia mara mbili kwenye kufuru hiyo. Wengine waliofunga ni kama inavyojieleza, Ba (31), Terry (45+1), Traore (50)

WAKATI HUOHUO....................

Wachezaji Juan Mata na Torres, huenda wakakosa mchezo wa kufungua ligi ya Uingereza kutokana na kukabiliwa na majukumu ya timu yao ya taifa ya Hispania, timu ya taifa ya Hispania itakuwa na mchezo wa kupimana nguvu siku tatu kabla ya mechi ya kuanza ligi kuu ya Uingereza.


Hakuna maoni:

Chapisha Maoni