Jumatano, 24 Julai 2013

NATAKA KUHAMIA ARSENAL asema SUAREZ
Mshambuliaji hatari wa klabu ya liverpool Luis Suarez amesema yuko tayari kuilazimisha klabu yake kumpa uhamisho ili ajiunge na klabu ya Arsenal. Mchezaji huyo ambaye mkataba wake unamruhusu kufanya hivyo kama tu timu itakayomtaka itaweza kufikia kiasi cha yuro milion 45.6, ameamua kutamka hayo baada ya klabu ya Arsenal kuwa tayari kulipa kias cha yuro milioni 49 kama ada ya uhamisho kwa mchezaji huyo lakini kocha wake amekataa kukubali kiasi hicho cha fedha akidai kwamba Suarez ana thamani sawa na mshambuliaji wa PSG Edson Cavani yaani yuro milioni 63 alizonunuliwa kutoka klabu ya Napoli ya Italia wiki iliyopita. Hata ivyo mshambuliaji huyo wa Liverpool amecheza mechi ya kupimana nguvu akitokea benchi na kutoa pasi ya goli la pili na la ushindi kwa timu hiyo. Suarez amesema ataiandikia Liverpool ili ilazimike kumuuza mchezaji huyo huku klabu ya Arsenal tayari ikijiamini kuwa ndiyo inategemea kumpata mshambuliaji huyo wakati wowote. Lakini wachambuzi wengi wa soka watashangaa sana iwapo klabu ya Arsenal itafanikiwa kumnasa mchezaji huyo kwani hapo awali alishaviponda vyombo vya habari vya Uingereza akidai vinamuharibia maisha yake hapo Uingereza kwahiyo hatokuwa tayari kusalia nchini humo. Ikumbukwe kwamba pia klabu kongwe ya nchini Hispania nayo inamuhitaji mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 26 raia wa Uruguai.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni