PATA HABARI MUHIMU KUTOKA VISIWA VYA ZIWA VICTORIA PAMOJA NA HABARI ZA MICHEZO ZA KIMATAIFA
Jumatano, 24 Julai 2013
NDOTO ZA ARSENAL KUMSAJILI HIGUAN ZAFIKIA MWISHO...........
Klabu ya Napoli ya Italia imekubaliana na mshambuliaji wa Real Madrid Gonzalo Higuan kumlipa kiasi cha yuro 163,000 kwa wiki hii ikiwa ni baada ya makubaliano kati ya vilabu hivi viwili kukubaliana ada ya uhamisho kiasi cha yuro milion 37. Mchezaji huyo atasaini mkataba wa miaka 5 wenye thamani ya yuro milioni 42.3 kwa mshahara wa miaka 5 tu. Ikumbukwe kwamba klabu ya Arsenal ndiyo walionekana kuwa na nafasi kubwa ya kumnasa mshambuliaji huyo raia wa Ajentina, lakini walishindwa kuafikiana ada ya uhamisho wa mshambuliaji huyo. Arsenal walikwisha kubaliana na Higuan mwenyewe lakini wakashindwa kufikia dau la yuro milioni 30 ambalo Real Madrid walitaka kama ada ya uhamisho. Kwa sasa klabu ya washika bunduki wa London wamehamishia nguvu zao kwa mshambuliaji wa kimataifa wa Uruguai Luis Suarez, ambapo mpaka sasa wako tayari kulipa ada ya uhamisho wa mchezaji huyo kiasi cha yuro milioni 49, hata hivyo klabu inayommiliki haijawa tayari kupokea kitita hicho.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni