ARSENAL YAONGEZA KITITA KUMNASA SUAREZ mil 49!
Klabu ya Arsenal ya jijini London, imeamua kupandisha dau lake ili kumnasa mshambuliaji hatari wa klabu ya Liverpool Luiz Suarez. Baada ya kuonekana kuzidiwa kete kwenye soko la wachezaji jioni hii baada ya mchezaji aliyetegenewa kutua kwenye viwanja vya Emirates muajentina Higuan kukaribia kabisa kumwaga wino kwenye klabu ya Napoli ya Italia, washika mtutu hao wa London wameamua kutoa dau la kiasi cha Yuro milion 49 ili kuipata huduma ya mshambuliaji kutoka Uruguai kijana machachari Luis Suarez. Ikionekana kabisa kuwa imedhamiria kumchukua mchezaji huo, klabu ya Arsenal imepanda dau hilo ili kumshawishi mshambuliaji huyo kuona kwamba haikuwa inatania pale ilipotangaza dau la Yuro milion 30 awamu ya kwanza kabla ya kutupiliwa mbali kabisa na Liverpool, hata ivyo klabu ya Liverpool haiko tayari kumuuza mchezaji huyo kwa dau ambalo haitarizika nalo. Ikumbukwe kwamba kocha wa Liverpool amekwisha tamka kwamba mchezaji wake huyo ana thamani sawa na aliyekuwa mshambuliaji wa Napoli Edsoni Cavani ambaye amenunuliwa na klabu ya PSG ya Ufaransa kwa kitita cha Yuro milioni 63, hivyo kufanya mbio za mfaransa Arsene Wenger kuwa ngumu kumpata mshambuliaji huyo ambaye bado anatumukia adhabu ya kukosa mechi 6 za mwanzoni mwa ligi kuu ya Uingereza. Hata ivyo mshambuliaji huyo a meshaonyesha nia ya kuihama klabu hiyo ili acheze katika mashindano ya vilabu bingwa barani ulaya. Katika mkataba wake wa awali, unaonyesha Suarez anaruhusiwa kuhama pale tu klabu itakayomtaka ikifika dau la Yuro milioni 46.5, lakini kocha wa Liverpool amesema hatokuwa tayari kupelekeshwa na mchezaji huyo ili amuuze. Ikumbukwe kuwa klabu tajiri duniani ya Real Madrid nayo inamnyemelea kwa karibu kabisa kijana huyo mwenye umri wa miaka 26.WAKATI HUOHUO
Raisi wa klabu kongwe ya Real Madrid Florentino Perez ametangaza kuwa hajapokea ofa yoyote ya kumtaka mchezaji Christian Ronaldo lakini ametanabaisha kwamba mchezaji huyo atastaafu akiichezea klabu hiyo tajiri duniani, pamoja na tetesi nyingi zinazomhusisha Ronaldo kurudi klabu yake ya zamani ya Manchester United pamoja na matajiri wa PSG kuonekana kumtaka kwa udi na uvumba, Perez amesema winga huyo mwenye umri wa miaka 28 atastaafu soka akiichezea Real Madrid ya nchini Hispania.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni