Jumatano, 24 Julai 2013

KLABU YA VALENCIA IKO TAYARI KUMUUZA MSHAMBULIAJI WAKE SOLDADO KWA TOTTENHAM....
Klabu ya Valencia ya nchini Hispania iko tayari kumuuza mshambuliaji wake hatari Soldado kwa timu ya Uingereza kama tu watafikia kiwango cha ada ya uamisho kiasi cha Yuro milioni 30 sawa na paundi milioni26, kwa muda mrefu sasa klabu ya Tottenham imekuwa ikimuwania mchezaji huyo wa kimataifa wa Hispania. Raisi wa klabu ya Valencia  Amadeo Salvo amesema wako tayari kumruhusu mchezaji huyo kuhama kama tu timu inayomtataka itafika dau hilo. Mtaalamu wa benchi la ufundi kutoka klabu ya Tottenham Flanco Baldini alikwenda nchini Hispania ili kumaliza suala la kumnasa mshambuliaji huyo, lakini klabu hiyo ilikataa kupunguza dau hilo. ''hatukuwa na mpango wa kumuuza mshambuliaji wetu huyu, lakini kama mtafika dau hatunabudi kumuuza'' alisema rais wa klabu ya Valencia.

Kocha Villa Boas akiongea na waandishi wa habari wa Hong Kong alisema wanahitaji huduma ya mshambuliaji huyo mwenye umri wa miak 28.


KLABU YA CHELSEA YAKATAA KUMUUZA MATA.....

Klabu ya matajiri wa London Chelsea, imepuuza maneno yanayosemwa kwamba inataka kumuuza mchezaji wake Juan Mata. Kumekuwa na tetesi kuwa mchezaji huyo atauzwa kwa klabu ya Barcelona au atawekwa kwenye mauziano kwa mabadilishano na mchezaji hatari wa Manchester United Wayne Rooney. Kwa msisitizo zaidi klabu hiyo ya darajani imeamua kuandaa mkataba mnono ili kumuongezea mshahara mchezaji huyo kutoka paundi 70,000 kwa wiki mpaka 100,000 kwa wiki, mkataba utakaomkalisha darajani mpaka mwaka 2018. Mchezaji huyo aliyetua darajani miaka 2 iliyopita akitokea Hispania kwenye klabu ya Valencia, alionekana kutokuwa kipenzi cha kocha Jose Mourinho. 

WAKATI HUOHUO ................................

Kocha mwenye maneno mengi, Jose Mourinho amesema yuko tayari kuisaidia timu ya taifa ya Uingereza ili ifanikiwe kufuzu fainali za kombe la dunia zitakazofanyika nchini Brazil mwakani. ''Nitawaandaa wachezaji wangu wa Uingereza ili wawe vizuri kwa ajili ya kuiweka timu yao kwenye mazingira mazuri ya kushiriki kombe la dunia mwakani'' alisema Mourinho, kocha huyo anayependa kuongea mara kwa mara ametaabanisha kwamba wachezaji wake raia wa Uingereza atawapa nafasi kikosini ili wapate uzoefu zaidi.

KATIKA HALI NYINGINE...................  

Mreno Jose Mourinho ametanabaisha kwamba klabu yake ya Chelsea haiko kwenye shinikizo kubwa la kutwaa ubingwa msimu huu kama walivyo Manchester City, ''wenzangu wamekwishatumia zaidi ya paundi milioni 100 kwenye usajili ili wabebe kombe'' alisema mwalimu huyo na kusema timu yenye kikosi bora kwa aonavyo yeye ni kikosi cha Pellegrini.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni