PATA HABARI MUHIMU KUTOKA VISIWA VYA ZIWA VICTORIA PAMOJA NA HABARI ZA MICHEZO ZA KIMATAIFA
Jumanne, 23 Julai 2013
CHELSEA WASAJILI KINDA KUTOKA CHILE
Klabu ya Chelsea yenye makazi yake katika jiji la London, imemsajili kinda mwenye umri wa miaka 18 kutoka kwenye klabu iitwayo O'Higgns ya nchini Chile, Christian Cuevas ni mchezaji mwenye uwezo wa kucheza kama beki wa kushoto na winga wa kushoto, ameshiriki katika mashindano ya kombe la dunia kwa vijana wenye umri wa chini ya miaka 20 yaliyomalizika hivi karibuni, mchezaji huyu ambaye anakuwa wa nne kusajiliwa msimu huu, amesaini mkataba utakaomkalisaha darajani mpaka mwaka 2018. Wachezaji wengine ambao tayari wamekwisha mwaga wino kwenye klabu hii tajiri ni Andre Schurrle kutoka Bayer Leverkusen, Marco Van Ginkel kutoka Vitesse na mchezaji huru Mark Schwarzer
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni